Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mhe. Kanali Aggrey John Magwaza amezindua shule ya Msingi Nyaruhaza.
Ujenzi wa Shule hiyo ulianza mwaka jana na kukamilika mwanzoni mwa mwaka huu.
Shule hii imejegwa kwa gharama ya shilingi million mia mbili na hamsini(250,000,000) toka Serikali kuu.
Katika uzinduzi huo Mhe. Mkuu wa Wilaya alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa kipaumbele katika suala zima la elimu hapa nchini.
Shule hii itasaidia kuondoa msongamano katika shule za msingi za Boma, Kibondo na Mapinduzi hivyo kuwezesha wanafunzi kujifunza kwa uzuri zaidi,
KIBONDO DISTRICT COUNCIL, KIBONDO TOWNSHIP IHULILO STREET
Anuani ya Posta: P.O.BOX 43, KIBONDO
Simu ya Mezani: +255 028 282 0084
Simu: +255 028 282 0084
Barua pepe: ded@kibondodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Kibondodc .Haki zote zimehifadhiwa.