• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua pepe za Ofisini |
KIBONDO DISTRICT COUNCIL
KIBONDO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serilali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Msingi wa Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Division ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Division ya Elimu Awali na Elimu Msingi
      • Division ya Elimu Sekondari
      • Division ya Huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Division ya Maendeleo ya Jamii
      • Division ya Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Division ya Kilimo Mifugo na Uvuvi
      • Division ya Viwanda Biashara na Uwekezaji
      • Division ya Mipango na Uratibu
      • Division ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
    • Vitengo
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Usafi na Usimamizi wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Afya, Elimu na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Elimu ya Msingi

1.0: UTANGULIZI.

Idara ya Elimu Msingi ni mojawapo kati ya Idara zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo. Idara hii ina vitengo vinne ambavyo vinaongozwa na Wakuu wa Vitengo ambao wanamsaidia Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku. Vitengo hivyo ni Elimu ya Watu Wazima, Taaluma, Vifaa na Takwimu na Utamaduni.

Kazi na majukumu ya kila kitengo yamefafanuliwa vizuri katika taarifa hii sehemu ya vitengo vilivyopo kwenye Idara. Ikumbukwe kwamba Idara ya Elimu Msingi ni moja ya Idara kubwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, hivyo majukumu yake ni mtambuka ambayo yanagusa Idara nyingine kama vile, Afya, Maji, Maendeleo ya Jamii, Kilimo na Mazingira.

Idara inafanya shughuli zake kwa kufuata sheria, kanuni, miongozo na taratibu zilizowekwa na OR - TAMISEMI na Serikali Kuu kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata Elimu bora itakayowawezesha kufaulu mitihani yao na kumudu maisha yao ya kila siku katika nyanja mbalimbali. Idara ina Watumishi ambao wanaweza kutimiza malengo yaliyowekwa na Idara endapo watasimamiwa na kuwepo mazingira ya kufundishia ikiwemo miundombinu mfano, Vyumba vya Madarasa, Madawati, na Matundu ya Vyoo.

IDADI YA SHULE ZA MSINGI

Na

Kata

Idadi ya Shule

Umiliki

Serikali

Binafsi

1
Bitare

4

4


2
Biturana

4

4


3
Bunyambo

5

5


4
Busagara

5

5


5
Busunzu

7

7


6
Itaba

4

4


7
Kagezi

3

3


8
Kibondo Mjini

5

5


9
Kitahana

4

4


10
Kizazi

5

5


11
Kumsenga

3

3


12
Kumwambu

5

4

1

13
Mabamba

7

7


14
Misezero

4

4


15
Mukabuye

3

3


16
Murungu

3

3


17
Nyaruyoba

5

5


18
Rugongwe

6

6


19
Rusohoko

5

5


JUMLA

87

86

1

 

MAAFISA WA IDARA YA ELIMU MSINGI WILAYA

Na

Jina la Mtumishi

Cheo

Namba za Simu

1
Mwl. Jamhuri O. Kidumu
Mkuu wa Idara

0754659201

2
Mwl. Winstone N. Msuya
Afisa Elimu Taaluma

0769970020

3
Mwl. Fatuma R. Mbano
Afisa Elimu Taaluma

0765245151


Mwl. Mohamedi M. Namtimba
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu

0757759856

4
Mwl. Filbert T. Misuzi
Afisa Elimu Watu Wazima

0756527490

5
Mwl. John N. Katunzi
Afisa Utamaduni

0769072368

6
Mwl. Amina J. Muliro
Afisa Elimu Vielelezo

0766250744

7
Mwl. Gaspar G. Kulikiza
Afisa Elimu Ufundi

0756892014

8
Mwl. Agnes O. Malinzi
Afisa Elimu Sayansi Kimu

0769482024

9
Mwl. Oliver G. Geofrey
Afisa Elimu Maalum

0769565154

10
Mwl. Gregory G. Nzuguru
Kaimu Afisa Michezo

0753520439

11
Bw. Optatus Kalungwana
Dereva

0758540321

12
Bw. Raphael Manangara
Mhudumu

0745216344

 

5.0 MAJUKUMU YA JUMLA YA IDARA

Idara ya Elimu Msingi ina majukumu mengi ambayo yanasaidia katika utoaji wa elimu bora, kwa ujumla yafuatayo ni majukumu ya Idara ya ElimuMsingi Wilaya;

  1. Upanuzi na uimarishaji wa Elimu Msingi
  2. Kuendesha mafunzo ya utunzaji na usimamizi wa fedha kwa kamati za shule, walimu na wanafunzi.
  3. Kusimamia wajibu, haki na maslahi ya walimu
  4. Kukusanya takwimu za shule za Msingi na kuzihifadhi, kuzitumia na kutuma kule zinakohitajika, mfano Ofisi ya RAIS TAMISEMI, WEST nk.
  5. Kufanya maandalizi kwa ajili ya watahiniwa wa Madarasa yanayofanya mitihani ya kitaifa na kuratibu mitihani yote ya Kitaifa kwa Shule za Msingi.
  6. Kufuatilia taarifa za ukaguzi wa shule ya msingi.
  7. Kufuatilia uhai wa kamati za shule na ununuzi wa vifaa vya shule.
  8. Kusimamia mafunzo ya walimu kazini katika ngazi zote; Astashahada, Stashahada na Shahada.
  9. Kuratibu na kusimamia mpango wa EWW, MUKEJA na MEMKWA
  10. Kuhakikisha kuwa fedha zote zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya shule yaani, Capitation Grant na Development Grant zinatumika kwa wakati na kufuatilia matumizi sahihi ya fedha hizo.
  11. Kutekeleza maagizo mbali mbali kutoka ngazi za juu kwa wakati.
  12. Kufanya tathmini ya mitihani mbalimbali inayofanyika,mfano; ya kiwilaya, kimkoa na kitaifa ili kubaini mafanikio na mapungufu ya Mtaala na kuchukua hatua pale inapogundulika kuwa kuna udhaifu.
  13. Kusimamia na kufuatilia masuala yote ya mtambuka.
  14. Kusimamia na kuratibu zoezi zima la michezo mashuleni.

MALENGO YA IDARA

  • Kuandikisha watoto wenye umri wa kwenda shule na kuwa na darasa la awali katika kila shule.
  • Kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanajua kusoma, kuandika na kuhesabu
  • Kupunguza idadi ya wanafunzi wanaoacha shule kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo mimba na utoro.
  • Kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la nne na darasa la saba katika mitihani yao.
  • Kuanzishwa vituo vya MEMKWA katika shule mbalimbali ili kuwapatia Elimu watoto waliokosa Elimu katika Mfumo rasmi
  • Kufuatilia ufundishaji katika shule zote zilizopo katika halamashauri ili kuona kama walimu:-
  • Wanajiandaa kabla ya kuingia darasani
  • Wanaingia darasani na wanafundisha
  • Wanatoa mazoezi ya kutosha kwa wanafunzi
  • Wanafanya tathimini ya ufundishaji
  • Kuwa na uongozi wa shule ulio imara wenye uwezo wa kusimamia ufundishaji, nidhamu, ya Walimu na Wanafunzi na unaoshirikiana na Kamati ya Shule na jamii kwa ujumla katika maswala yanayohusu shule kama vile. Vikao, mapato ya shule, miradi ya miundombinu na mipaka ya shule.
  • Kukuza vipaji vya wanafunzi katika fani za utamaduni na michezo kwa kusimamia shughuli za utamaduni kama vile, ngoma, nyimbo, mashairi, ngonjera, maigizo na michezo mbalimbali inayofanyika katika shule zote.
  • Kila shule kuwa na mradi wa Elimu ya kujitegemea ambao utaongeza mapato ya shule na uhifadhi wa mazingira.
  • Kuwahudumia walimu na wananchi kwa usawa na kwa haraka wanapokuwa na mahitaji ya kuhudumiwa na Ofisi ya Elimu kama vile, uhamisho wa wanafunzi, ruhusa, ugonjwa na vifo, kujibu barua za walimu kwa haraka, kupitisha mihtasari ya matumizi ya fedha za shule, kusikiliza shida na matatizo ya walimu na kuwathamini.
  • Kutoa motisha kwa Walimu na Shule zilizofanya vizuri katika taaluma, michezo, usafi na utunzaji wa mazingira.
  • Kuwa eneo lisilopokea rushwa (Curruption Free Zone) ambapo huduma itatolewa kwa haki bila upendeleo, kwa haraka na bila usumbufu.
  • Kushirikiana na wadau wa kisekta kama vile, Idara ya Elimu Sekondari, Uthibiti Ubora wa Shule, Tume ya Utumishi wa Walimu na Chama cha Walimu Tanzania katika kusimamia utoaji wa Elimu bora na huduma bora kwa Walimu.
  • Kila mdau wa Elimu anapata taarifa za Idara ya Elimu bila vikwazo kwa usahihi na haraka zinapohitajika.

 

 

 

4.0: VITENGO VYA IDARA NA MAJUKUMU YAKE

Kama ilivyoelezwa katika utangulizi wa taarifa hii idara ina vitengo vinne (4) ambavyo ni.

Elimu ya Watu Wazima ambayo ndani yake kuna vitengo vidogo vitano (5) ambavyo ni Vielelezo, Ufundi, Kilimo, Sayansi Kimu na Elimu Maalum, Kitengo cha Taaluma, Kitengo cha Vifaa na Takwimu na Kitengo cha Utamaduni na Michezo.

MAJUKUMU YA AFISA ELIMU WATU WAZIMA WILAYA

  • Msaidizi wa Afisa Elimu Wilaya /Halmashauri kuhusu Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi (EWW/ENMRA)
  • Mshauri mkuu wa Afisa Elimu Wilaya /Halmashauri kuhusu Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi (EWW/ENMRA) katika Wilaya.
  • Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi katika Wilaya/Halmashauri
  • Kuandaa bajeti ya mahitaji ya kitengo cha Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi (EWW/ENMRA) katika wilaya ikiwemo mishahara ya watumishi , posho za wawezeshaji /walimu wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi.
  • Kubuni mipango ya kuendeleza taaluma ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi yanayoendeshwa katika wilaya.
  • Kuratibu mashindano ya kitaaluma ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi (EWW/ENMRA) yanayaoendeshwa katika Halmashauri.
  • Kuandaa mahitaji na ugawaji wa raslimali zihusuzo Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi (EWW/ENMRA)
  • Kukusanya kuchanganua na kutayarisha taarifa za Utekelezaji wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi (EWW/ENMRA) katika wilaya na kuziwasilisha katika ngazi zote.
  • Kuandaa mafunzo kwa watekelezaji wa Elimu ya Watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi (EWW/ENMRA) katika ngazi ya Wilaya.
  • Kuratibu Shuguli zote za Elimu ya watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi (EWW/ENMRA) zinazoendeshwa na Wizara,Taasisi,mashirika ya Umma na ya Watu binafsi katika Wilaya na kutoa taarifa.
  • Kuratibu utoaji wa Elimu masafa na ya ana kwa ana kwa kushirikiana na mkufunzi mkazi wa taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoa na waratibu wa vituo katika Sekondari na Vyuo.
  • Kuratibu utoaji wa Elimu ya Sekondari katika vituo vya ufundi stadi na vya watu binafsi nje ya Mfumo rasmi
  • Kuraibu mipango ya kufuta ujinga wa kutojua kusoma kuandika na kuhesabu inavyoendeshwa na shule za sekondari
  • Kupokea taarifa zaukaguzi wa madarasa na shughuli mbalimbali za Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi (EWW/ENMRA) na kufuatilia utekelezaji wa maamuzi.
  • Ni kiungo cha upashanaji wa habari za mipango ya kielimu kati ya Kata, Taasisi, Mashirika ya Umma na watu binafsi katika Wilaya/Halmashauri
  • Kuendesha mikutano na warsha za kuhamasisha viongozi wa Wilaya, Kata, Vijiji wananchi kuhusu masuala ya Elimu kwa ujumla.
  • Kusimamia maadhimisho ya juma la Elimu ya Watu wazima na juma la Elimu kwa wote katika Wilaya.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopewa na Mkuu wake wa kazi.

 

 MAJUKUMU YA AFISA ELIMU VIELELEZO WA WILAYA 

  1. Kusimamia upatikanaji wa vielelezo katika utoaji wa Elimu ya Msingi, Sekondari, Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi.
  2. Mshauri wa Afisa Elimu wa Msingi, Sekondari, Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi kuhusu masuala ya vielelezo vya elimu katika Halmashauri.
  3. Kuandaa na kutunza kumbukumbu zote muhimu kuhusu Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi.
  4. Kusimamia taaluma ya uandishi wa vitabu vya kiada, ziada, magazeti na nakala mbalimbali kwa ajili ya Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi katika Halmashauri
  5. Kushirikiana na Afisa Elimu Taaluma wa Msingi na Sekondari kuandaa vielelezo mbalimbali vya kuboresha ufundishaji wa masomo ya elimu ya msingi sekondari Elimu ya watu wazima nje ya Mfumo rasmi.
  6. Kushirikiana na Afisa Elimu Taaluma wa Msingi na Sekondari mhariri wa magazeti vijijini wa kanda katika kuandaa na kuendesha mafunzo kwa njia ya filamu, video, Tv, Mabango na vipeperushi.
  7. Kupokea, kuhifadhi na kusambaza vifaa vyote vya Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi katika Halmashauri
  8. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi

 

 MAJUKUMU YA AFISA ELIMU UFUNDI WA WILAYA

  1. Mshauri wa Afisa Elimu wa msingi ,sekondari na Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi kuhusu masuala ya elimu ya ufundi katika Halmashauri
  2. Kusimamia elimu ya ufundi katika shule za msingi na sekondari vituo vya elimu ya watu wazima na elimu nje ya Mfumo rasmi
  3. Kuandaa makadirio ya matumizi ya fedha kwa ajili ya kutekeleza mipango ya ufundi katika shule za msingi na Sekondari na Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi ili yaingizwe katika bajeti ya Halmashauri
  4. Kuratibu mipango yote ya elimu ya ufundi iliyoendeshwa na wizara taasisi mashirika ya umma ya kijamii na watu binafsi.
  5. Kuratibu uendeshaji wa miradi ya ufundi ya uzalishaji mali katika shule za sekondari vituo vya elimu ya watu wazimu nje ya Mfumo rasmi shule za ufundi stadi na msingi kwa kushirikiana na shirika la SIDO.
  6. Kuhakikisha usalama kusimamia uendeshaji wa mitihani ya ufundi stadi katika Halmashauri.
  7. Kuteua na kupanga walimu wa ufundi katika vituo vya shule kwa kushirikiana na Afisa Elimu Msingi na Sekondari.
  8. Kushirikiana na Afisa Elimu vifaa na Takwimu Mratibu wa Elimu maalum na Mhandisi Wilaya kuhakikisha ujenzi wa madarasa nyumba za walimu na vyoo na majengo mengine ya shule yanajengwa kwa kufuata vipimo sahihi vinavyotolewa na Wizara na Elimu na mafunzo ya ufundi.
  9. Kutayarisha taarifa ya utekelezaji wa elimu ufundi ya kila robo mwaka, nusu na mwaka mzima na kuziwasilisha katika sehemu zote zinzohusika.
  10. Kusimamia ufunguzi wa vituo vya ufundi na sekondari kulingana na mwongozo wa Wizara.
  11. Kushirikiana na Afisa Elimu Taaluma msingi na sekondari kuandaa na kuendesha mafunzo ya kujenga uwezo wa walimu wa ufundi katika ngazi ya Wilaya.
  12. Kufuatilia taarifa za ukaguzi wa shughuli za ufundi katika shule za Msingi, sekondari na vituo vya Elimu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi.
  13. Kupokea na kuweka takwimu sahihi za idadi ya wanafunzi walimu na wafanyakazi wasio walimu wa shughuli za ufundi katika shule za msingi, Sekondari, vituo vya Elimu ya watu wazima na Elimu ya nje ya Mfumo rasmi.
  14. Kuhamasisha wenye taaluma ya ufundi kujiunga na mafunzo ya elimu ya ufundi kwa lengo la kupata waalimu wataalamu

 

 

 

 

 

MAJUKUMU YA AFISA ELIMU SAYANSI KIMU WA WILAYA.

  1. Mshauri wa Afisaelimu Msingi, Sekondari na Elimu ya Watu Wazima kuhusu masuala ya elimu ya Sayansi Kimu na Afya katika Halmashauri.
  2. Kusimamia elimu ya sayansi kimu na afya katika shule za msingi, sekondari, elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi
  3. Kuratibu shughuli zote za afya na lishe katika shule za msingi, sekondari na vituo vya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi.
  4. Kuandaa makadirio ya matumizi ya fedha kwa ajili ya kutekeleza mipango ya sayansi kimu na afya katika shule za msingi, sekondari na vituo vya EWW nje ya mfumo rasmi ili yaingizwe katika mipango na bajeti za Halmashauri.
  5. Kushirikiana na Afisaelimu Taaluma Msingi na Sekondari kutoa ushauri na kuandaa mafunzo kwa walimu wanaofundisha somo la sayansi kimu na afya katika shule za msingi, sekondari na vituo vya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi.
  6. Kutoa ushauri nasaha na unahisi kwa walimu, wazazi na wanafunzi kuhusu afya ya uzazi, malezi bora na tabia njema.
  7. Kuanzisha vituo vipya vya sayansi kimu na afya katika shule za msingi na sekondari na kushauri namna ya kuviendesha kufuatana na mwongozo wa Wizara.
  8. Kutafuta na kusimamia usambazaji wa vifaa vyote vya sayansi kimu na afya katika shule.
  9. Kutayarisha taarifa za utekelezaji wa elimu ya sayansi kimu na afya ya kila robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima na kuziwasilisha katika sehemu zote zinazohusika.
  10. Kushirikiana na watendaji wa sekta ya afya, maji, maendeleo ya jamii, ustawi wa jamii pamoja na mashirika ya kijamii katika kuendeleza elimu ya sayansi kimu na afya katika shule za msingi na sekondari.
  11. Kuhamasisha wenye taaluma ya sayansi kimu na afya kujiunga na mafunzo ya elimu ya sayansi kimu na afya kwa lengo la kupata walimu wataalamu.
  12. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

 

MAJUKUMU YA KITENGO CHA ELIMU MAALUM

  1. kubainisha wanafunzi wenye ulemavu na mahitaji maalum na kuhifadhi kumbukumbu.
  2. Kubainisha walimu wenye ulemavu na kuhifadhi zao
  3. Kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji maalum na walemavu wanasajiliwa kufanya mtihani.
  4. Kusimamia na kuhakikisha kuwa huduma kwa wanafunzi walemavu na wenye mahitaji maalum zinapatikana kwa wakati.
  5. Kushirikiana na Afisa Elimu vifaa na Takwimu kupata takwimu sahihi za wanafunzi wenye ulemavu.
  6. Kuandaa na kutuma taarifa za kila robo za wanafunzi wenye mahitaji maalum na walemavu.
  7. kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

MAJUKUMU YA KITENGO CHA TAALUMA

  1. Kupanga, kuratibu na kusimamia taaluma katika Wilaya.
  2. Kufuatilia ufundishaji katika shule za msingi na kusimamia Mtaala wa Elimu.
  3. Kukusanya takwimu za watahiniwa wa darasa la IV na VII kutoka shuleni kuzihakiki na kuziwasilisha Mkoani kila mwaka.
  4. Kufuatilia taarifa za ukaguzi wa elimu ya msingi.
  5. Kufuatilia na kutoa ushauri kwa walimu juu ya utekelezaji wa mitaala ya elimu na mihtasari.
  6. Kupanga, kuratibu na kusimamia uendeshaji wa mitihani ya darasa la IV na VII ya Wilaya, Mkoa na Taifa kila mwaka.
  7. Kutathimini mitihani ya darasa la IV na VII ili kubaini mafanikio na udhaifu na kurekebisha mapungufu.
  8. Kupanga na kuendesha semina kwa Walimu Wakuu, Walimu Wakuu Wasaidizi na Waratibu Elimu Kata.
  9. Kufuatilia utoro wa walimu katika vituo vya kazi.
  10. Kuanzisha na kuhimiza matumizi bora ya vituo vya walimu TRC
  11. Kutekeleza maagizo yote kutoka ngazi za juu.

 

MAJUKUMU YA KITENGO CHA VIFAA NA TAKWIMU

  1. Kukusanya, kuchambua, kufafanua, kuhifadhi, kutoa na kupokea takwimu za elimu ya msingi na kuziwasilisha zinakohitajika bila kuchelewa.
  2. Kufuatilia na kusimamia upanuzi na uimarishaji wa shule za msingi.
  3. Kufanya makisio ya idadi ya walimu kwa madaraja, kufuatana na upungufu na upanuzi.
  4. Kufanya makisio ya miundombinu na samani za shule zinazohitajika kulingana na idadi ya watumiaji.
  5. Kuratibu shughuli za Uagizaji na usambazaji wa vifaa vya shule kulingana na mahitaji ya shule na fungu la fedha.
  6. Kusimamia matumizi ya fedha kulingana na mahitaji, kwa kufuata kanuni na miongozo inayotolewa na Wizara.
  7. Kushirikiana na maafisa wengine kutoa huduma muhimu ikiwemo kusimamia mahudhurio ya walimu na wanafunzi, uhamisho na kuhamasisha jamii /shule kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi.
  8. Kufanya makisio ya bajeti ya Idara kulingana na mahitaji kwa kuzingatia miongozo inayotolewa.
  9. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

 MAJUKUMU YA KITENGO CHA UTAMADUNI

  1. Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Sera ya Utamaduni, Sera ya michezo na sera ya mfuko wa Utamaduni katika ngazi ya wilaya.
  2. Kutoa ushauri juu ya uendeshaji wa utamaduni na michezo katika asasi mbalimbali katika ngazi ya wilaya.
  3. Kuratibu shughuli zote za maendeleo ya utamaduni na michezo katika wilaya.
  4. Kuwa msajili msaidizi wa vikundi vya sanaa ,vilabu vya michezo na vyama vya michezo katika wilaya.
  5. Kutoa ushauri nakufuatilia utekelezaji wa uhakika juu ya matumizi sahihi ya lugha ya Taifa (Kiswahili) katika wilaya.
  6. Kutambua na kuhifadhi maeneo mbalimbali ya kihistoria, makumbusho na nyaraka na matukio yanayojitokeza wilayani kwa ajili ya picha ,filamu na vitabu.
  7. Kutoa ushauri juu ya ujenzi na uendeshaji wa nadharia ya sanaa na majukwaa au kumbi zinazotumika kuonyeshea sanaa za maonyesho.
  8. Kufanya utafiti wa mila na desturi, fasihi simulizi ,sanaa za jadi na fani mbalimbali za michezo.
  9. Kushauri juu ya mitaala ya mafunzo ya sanaa,Lugha,michezo na tafsiri katika shule na vyuo mbalimbali vinavyohusika.
  10. Kuandaa na kuendesha warsha na mafunzo mbalimbali kwa vikundi vya sanaa na vikundi vya michezo ili kuweza kuwajengea uwezo kiutendaji.
  11. Kusimamia uendeshaji wa vituo vya sanaa,lugha na majukumu ya sanaa za maonyesho.
  12. Kudhibiti uonyeshaji wote wa maonyesho mbalimbali ya sanaa yakiwemo filamu,cinema na uuzaji wa kanda za video ili kulinda maadili ya jamii ya Taifa kwa jumla.
  13. Kuwa na utaratibu wa mahusiano wa sanaa na lugha kimataifa.
  14. Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu vipimo sahihi, uendeshaji na utunzaji wa viwanja vya michezo na maeneo ya burudani
  15. Kusimamia utekelezaji wa katiba na kanuni za vyama vya michezo katika wilaya.
  16. Kukusanya takwimu mbalimbali za utamaduni na michezo katika wilaya

Matangazo

  • KUITWA KWENYE MAFUNZO ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUSITISHA WITO WA USAILI April 27, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI May 05, 2023
  • BADILIKO LA TANGAZO LA KAZI May 05, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MADIWANI WA HALMASHAURI YA KIBONDO WAPONGEZWA JUU YA UTENDAJI KAZI WAO

    May 07, 2025
  • WAFANYAKAZI WAHIMIZWA KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025

    May 01, 2025
  • WANANCHI WA VIJIJI VYA RUGUNGA NA KITAHANA KATIKA KATA YA KITAHANA WATOA KERO ZAO KWA MKUU WA WILAYA KIBONDO

    March 21, 2025
  • KAMPENI YA UGAWAJI VYANDARUA YA ZINDULIWA KIBONDO

    March 15, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Constructions of Latrines
  • Investment Reports
  • Construction of Four Stall at Nanenane Bus Stand
  • Construction of Health Staff House at Kifura
  • Rehabilitation of Canteen at CotC Kibondo
  • Construction of Administration Building
  • OPRAS FOMU
  • Sick-Sheet Forms
  • Upimaji wa Viwanja Eneo la Kijiji cha Nengo

Zinazohusiana

  • UTUMISHI
  • PO-RALG
  • NECTA
  • PUBLIC PROCUREMENT REGULATORY AUTHORITY
  • UTUMISHI PORTAL
  • KIGOMA REGION
  • WANANCHI PORTAL
  • INVESTMENT CENTRE
  • AJIRA
  • Ministry of Industries

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Wasiliana nasi

    KIBONDO DISTRICT COUNCIL, KIBONDO TOWNSHIP IHULILO STREET

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 43, KIBONDO

    Simu ya Mezani: +255 028 282 0084

    Simu: +255 028 282 0084

    Barua pepe: ded@kibondodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma
    • Kanusho

Hakimiliki ©2017 Kibondodc .Haki zote zimehifadhiwa.