Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo imeanza mradi wa upimaji wa viwanja 1,500 vya makazi,biashara na huduma za kiuchumi na kijamii katika eneo la Nengo. Eneo hili liko katika Mamlaka ya Mji Mdogo Kibondo. Mara mradi utakapokamilika, utaratibu wa upatikanaji wa viwanja hivyo utatangazwa rasmi. Hata hivyo Menejimenti ya Halmashauri inaendelea kuwasisitiza wananchi ambao maeneo yao yatatwaliwa kwa ajili ya mradi huu kutoa ushirikiano wa kutosha ili kukamilisha mradi kwa wakati na kwa maendelea ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo.
KIBONDO DISTRICT COUNCIL, KIBONDO TOWNSHIP IHULILO STREET
Anuani ya Posta: P.O.BOX 43, KIBONDO
Simu ya Mezani: +255 028 282 0084
Simu: +255 028 282 0084
Barua pepe: ded@kibondodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Kibondodc .Haki zote zimehifadhiwa.