Mkuu wa Wilaya ya Kibondo ,he. Kanali Aggrey J. Magwaza ameshiriki maadhimisho
ya Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Maadhimisho hayo kiwilaya yamefanyika katika kijiji cha Kumkugwa kata ya Misezero.
Katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya alizungumza na wananchi wakazi wa Kata ya Misezero.
Baada ya kuongea na wananchi Mhe. Mkuu wa Wilaya alizindua barabara ilitengenezwa na wananchi wanaonufaika na Mpango wa TASAF.
Barabara hiyo ina urefu wa kilomita 2.2 toka barabara kuu la Kakonko - Kibondo ambayo imegharimu jumla ya Shilingii 19,294,000.
Barabara hiyo imejengwa ili kuhamisha barabara ya awali iliyokuwa ikipita katikati ya Shule ya Msingi Kumkugwa hivyo kupunguza umakini kwa wanafunzi
wakati wa masomo.
Vile vile Mkuu wa Wilaya alishiriki zoezi la upandaji miti, ambapo jumla ya miti 300 ilipandwa katika shamba la kijiji lenye miti 7,200.
Gharama za upandaji miti katika shamba hilo zimetolewa na Serikali kuu kupitia Mpango wa TASAF ambapo kiasi cha
Shilingi 13,759,000 zimetumika.
Mwisho Mkuu wa Wilaya alisikiliza kero za wananchi na kuacha maagizo kuwa zinazohusu utekelezaji zifanyiwe kazi haraka.
KIBONDO DISTRICT COUNCIL, KIBONDO TOWNSHIP IHULILO STREET
Anuani ya Posta: P.O.BOX 43, KIBONDO
Simu ya Mezani: +255 028 282 0084
Simu: +255 028 282 0084
Barua pepe: ded@kibondodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Kibondodc .Haki zote zimehifadhiwa.