Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo limeptisha bajeti ya kiasi cha Shilingi Billioni 34.0 kwa mwaka wa fedha 2023/2024. Kikao cha baraza la madiwani kimefanyika leo Alhamis tarehe 26 Januari 2023.
Wakichangia katika mjadala wa kikao hicho, Waheshimiwa madiwani walishauri kuimarishwa kwa ukusanyaji wa mapato kwa kuziba mianya ya upotevu na kuimarisha usimamizi.
Vile vile walipendekeza kuongezwa kwa vyanzo zaidi vya mapato ikiwemo kuanzisha uvuvi katika bwawa la Kilalangoma.
Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo imepanga kuongeza utoaji wa huduma za afya kwa kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Kizazi. Kituo hicho kimeanza kujengwa kwa nguvu za wananchi hivyo uongozi wa Halmashauri umetoa kipaumbele ujenzi huo ili kuunga juhudi nguvu za wananchi katika kuboresha huduma za afya.
Vile vile utoaji wa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu utaendelea kupewa kipaumbele. Kuimarika kwa mapato ya ndani kutaimarisha upatikanaji wa fedha nyingi Zaidi hivyo kupunguza changamoto ya ukosefu wa mitaji kwa wananchi wa Wilaya ya Kibondo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Henry Chinyuka aliahidi kuzingatia maoni yaliyotolewa na waheshimiwa madiwani katika kipindi chote cha utekelezaji wa bajeti hii ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Katika mkutano huo wa bajeti, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo aliahidi kuendelea kushirikiana na waheshimiwa madiwani, watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla ili kuleta maendeleo Zaidi.
Alisisitiza kuwa usalama utaendelea kuimarishwa na wananchi watakuwa na mazingira mazuri Zaidi ya kufanya kazi zao za kiuchumi.
KIBONDO DISTRICT COUNCIL, KIBONDO TOWNSHIP IHULILO STREET
Anuani ya Posta: P.O.BOX 43, KIBONDO
Simu ya Mezani: +255 028 282 0084
Simu: +255 028 282 0084
Barua pepe: ded@kibondodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Kibondodc .Haki zote zimehifadhiwa.