• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua pepe za Ofisini |
KIBONDO DISTRICT COUNCIL
KIBONDO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serilali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Msingi wa Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Division ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Division ya Elimu Awali na Elimu Msingi
      • Division ya Elimu Sekondari
      • Division ya Huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Division ya Maendeleo ya Jamii
      • Division ya Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Division ya Kilimo Mifugo na Uvuvi
      • Division ya Viwanda Biashara na Uwekezaji
      • Division ya Mipango na Uratibu
      • Division ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
    • Vitengo
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Usafi na Usimamizi wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Afya, Elimu na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MKUU WA MKOA WA KIGOMA AAGIZA KUFANYIWA KAZI MAAGIZO YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE-LAAC NA HOJA ZA CAG KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO.

Posted on: June 15th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (Msaafu) Mhe. Thobias E. M. Andengenye, ameagiza Viongozi na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge  - LAAC na Maoni ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali -CAG.

Ameyasema hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kilichofanyika jana (Tarehe:14/06/2023) katika ukumbi wa Halmashauri -IOM kujadili taarifa ya Ukaguzi wa CAG kwa Hesabu za Mwaka wa Fedha 2021/2022. Katika ukaguzi huo, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo ilipata hati safi (Unqualified) ikiwa ni miaka wa saba mfululizo.

Mhe. Mkuu wa Mkoa alitoa pongezi kwa Waheshimiwa Madiwani na Watendaji wa Halmashauri kwa kupata hati safi. Alisisitiza kuendelae kujibu hoja zilizoibuliwa na kuhakikisha hazijirudii tena. Alisema ni lazima sasa kuwa na utamaduni wa kuzuia hoja zisijitokeza.

Alisema katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya sita, miradi mingi imeletewa fedha hivyo ni muhimu kuwa na usimamizi makini na kuongeza uadilifu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akileta fedha nyingi. Tunamshukru sana na tunapaswa kudhihirisha hilo kwa kuwa na matumizi sahihi ili miradi iliyokusudiwa iweze kukamilika kwa wakati na kuleta matunda kwa wananchi.

Katika kikao hicho Katibu Tawala wa Mkoa Ndg. Albert Msovela alisema hatakuwa tayari kuona watumishi anaowasimamia wakikiuka maelekelezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa na Viongozi wa Serikali kwa ujumla. Atachukua hatua mara moja kwa mtumishi atakaye sabibisha hoja na kukiuka maadili ya utumishi.

Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mhe. Kanali Aggrey J. Magwaza alimwahidi Mkuu wa Mkoa kuwa ataendelea kusimamia maelekezo yote. Pia alimshukuru Rais wa Jamhuri, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Kibondo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Mhe. Habili C. Maseke alimshukru Mkuu wa Mkoa kwa kuhudhuria katika kikao hiki. Alisema yeye na Waheshimiwa Madiwani wataendelea kusimamia Halmashauri na kushirikiana na watumishi ili kuleta maendeleo zaidi. Hawatasita kuchukua hatua pale taratibu zitakapokiukwa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Ndg. Diocles M, Rutema alimwahidi Mkuu wa Mkoa na Viongozi wote kwa ujumla kuwa ataendelea kuwasimamia Watumishi wa Halmashauri. Atahakikisha taratibu zote zinafuatwa katika utekeleza wa miradi mbalimbali ya maendeleo na shughuli za kawaida zinazofanywa na watumishi. Ataendelea kusimamia nidhamu na uadilifu ili wananchi waendelee kupata huduma bora zaidi.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAPIGA KURA NJE YA KITUO ULICHOJIANDIKISHA September 15, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MABADILIKO June 17, 2025
  • MATOKEO YA USAILI KWA VITENDO MADREVA June 25, 2025
  • KUITWA KAZINI June 26, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAONESHO YA NANENANE YAWAPA FURSA WAKULIMA KUONGEZA TIJA

    August 08, 2025
  • MKUU WA MKOA TABORA AAGIZA UJENZI WA MABANDA YA KUDUMU KATIKA VIWANJA VYA NANENANE IPULI

    August 02, 2025
  • MKUU WA MKOA WA KIGOMA AWASISITIZA WATUMISHI WA KIBONDO KUWEKA MKAZO KWENYE UWEKEZAJI

    July 10, 2025
  • MKUU WA WILAYA KIBONDO AWAPONGEZA NA KUWAAGA WAHE. MADIWANI

    June 20, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Constructions of Latrines
  • Investment Reports
  • Construction of Four Stall at Nanenane Bus Stand
  • Construction of Health Staff House at Kifura
  • Rehabilitation of Canteen at CotC Kibondo
  • Construction of Administration Building
  • OPRAS FOMU
  • Sick-Sheet Forms
  • Upimaji wa Viwanja Eneo la Kijiji cha Nengo

Zinazohusiana

  • UTUMISHI
  • PO-RALG
  • NECTA
  • PUBLIC PROCUREMENT REGULATORY AUTHORITY
  • UTUMISHI PORTAL
  • KIGOMA REGION
  • WANANCHI PORTAL
  • INVESTMENT CENTRE
  • AJIRA
  • Ministry of Industries

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Wasiliana nasi

    KIBONDO DISTRICT COUNCIL, KIBONDO TOWNSHIP IHULILO STREET

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 43, KIBONDO

    Simu ya Mezani: +255 028 282 0084

    Simu: +255 028 282 0084

    Barua pepe: ded@kibondodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma
    • Kanusho

Hakimiliki ©2017 Kibondodc .Haki zote zimehifadhiwa.