Mkurugenzi Mtendaji(W) Ndg. Diocles Rutema leo tarehe 11/1/2022 amekabidhi madarasa 68 yaliyojengwa katika shule 15. Madarasa haya ni ya mradi wa mkakati wa Taifa wa kupambana na ugonjwa wa UVIKO-19. Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mhe. Kanali Aggrey J. Magwaza amekabidhiwa madarara haya ili naye akabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
Katika hafla hii ya makabidhiano Mkuu wa Wilaya aliwapongeza watendaji wa Serikali na wananchi waliojitoa kuhakikisha ujenzi huu unakamilika kwa wakati.
Pia aliwataka walimu kusimamia matumizi sahihi ya madarasa haya ili yaweze kudumu zaidi.
KIBONDO DISTRICT COUNCIL, KIBONDO TOWNSHIP IHULILO STREET
Anuani ya Posta: P.O.BOX 43, KIBONDO
Simu ya Mezani: +255 028 282 0084
Simu: +255 028 282 0084
Barua pepe: ded@kibondodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Kibondodc .Haki zote zimehifadhiwa.