Progarmu wa Shule Bora inaendeshwa katika Mikoa tisa ya Tanzania bara ambayo ni Kigoma, Mara, Simiyu, Singida, Dodoma, Katavi, Rukwa, Tanga na Pwani. Progamu hii itatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 01 Julai 2022 hadi 01 Julai 2027 chini ya ufadhiliwa na UKAID.
Progarmu ya Shule Bora inalenga kuboresha ufaulu kwa kujenga mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia. Matokeo mazuri darasani yanaweza kupatikana pale wanajamii watakapoona kuwa wanao wajibu wa kushiriki kikamilifu katika ujifunzaji kwa watoto wao. Hii itaondoa dhana kuwa shule ni mali ya Serikali na hivyo suala la usimamizi wa shule ni kwa walimu na viongozi wa elimu/shule tu.
Mafunzo ya Progarmu wa SHULE BORA kwa Maafisa Elimu Kata, Walimu wakuu na Wenyeviti wa kamati za shule yameanza leo tarehe 28/2/2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo.
KIBONDO DISTRICT COUNCIL, KIBONDO TOWNSHIP IHULILO STREET
Anuani ya Posta: P.O.BOX 43, KIBONDO
Simu ya Mezani: +255 028 282 0084
Simu: +255 028 282 0084
Barua pepe: ded@kibondodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Kibondodc .Haki zote zimehifadhiwa.