KATIBA YA KUDUMU YA 1977 YA TANZANIA,
UTUMWA NIKOSA LAJINAI.
Faini 50.000.000 Edina lutengano 0713975000
Biashara ya utumwa maana yake ni usafirishaji,uhifadhi,upokeaji,wa mtu au watu kwa njia ya kujia ya malipo, utekajinyara ,vitisho na ulaghai kwa lengo la unyonyaji.
Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 ibara 9 inasema Lengo la katiba hii nkuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya muungano na serikali ya mapinduzi Zanzibar au wa chochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana na kufuata siasa ya ujamaa nakujitegemea ambayo inasisitiz utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingati mazingira yaliyomo katika jamhuri ya muungano . kwahiyo mamlaka ya na vyombo vyake vyotenvinawajibika kuelekeza sera na shughuri zake zote katika lengo la kuhakikisha {c} kwamba shughuri za serikali zinatekelezwa kwanjia ambayzo zitahakikisha kwamba utajili wa Taifa unaendelezwa ,unahifaadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa ujumla na pia kumzuia mtu kumnyonya mtu mwingine.
{f} Kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishw kwa kufuata kanuni za tangazo la dunia kuhusu haki za binadamu. Hapo ndipo huwa napenda kutoa rai kwamba,
Tusipokua makini tutarudi ukoloni.
Rai yangu daima ni kuwataka Watatnzania wenyewe wamiliki uchumi kama hakikisho pekee kwamba maliasili yao na nguvu zao vinatumika kuwanaufaisha wananchi wanchi hii badala ya kunufaisha kundi la watu wachache hii ni kauri ya . Mh,Raisi John pombe Magufuri.
Miongoni mwa misemo yenye radha ambayo inarudisha matumaini kwa wa Tanzania ambayo imetolewa na utawala wa awamu ya tano kwa watanzania nikauri aliyotolewa na Mh;Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuri isemayo .Hakuna sababu ya pamba inayo limwa jinja (Uganda) iende ulaya kutengeneza nguo na ajira kwa vijana wao na nguo ambazo wanavaa wazungu wakizichoka wanazirejesha kwetu kama mitumba. Makala yangu inajikita katika mustakabari wa taifa letu ambalo hadi sasa limetimiza miaka yakujitawala kama taifa huru miaka (57)lakini wakati huo huo baadhi ya watanzania wenye mawazo ya kunyonya wenzao bado wa naratibu na wanasimamia biashara ya kuuza watanzania wenzao kwa ghiriba,utekaji na vitisho kwa tama ya kujipatia utajiri wa haraka haraka bila kujali madhara yanayo tokana na biashara hii ya utumwa kwa kutumia mbinu mpya, ,mtindo mpya na technologia mpya.Kabla sijaingia kwa undani kuzungumzia athari za utumwa nimeona itakuwa nivizuri kukutaarifu ndugu mtanzania mwenzagu kwamba tarehe 8.6.2018 hapa wilayani kibondo imefanyika semina ambayo imesaidia kuwaelimisha wahusika wa asasi zisizo za kiserikali ,taasisi mbalimbali za kiserikali na baadhi ya idara pia vitengo kutoka Halmashauri ya wilaya ya kibondo maana ya utumwa, unyonyaji na madhara yake kwa jamii. Kama alivyojitaja muendesha semina kwa majina mawili kwamba anaitwa EDINA LUTENGANO Na za simu 0713 975000 nakwamba anatoka katika asasi isiyo ya kiserikali iitwayo IOM .Lutengano amewafafanulia wanasemina hao kwamba,maana ya utumwa kama ilivyo fafanuliwa ndani ya Protocal ya umoja wa matifa utumwa niusaili,usafilishaji,uhifadhi,upokeaji wa mtu au kundi lawatu kwa njia ya vitisho, malipo .nguvu,utekaji nyara udanganyifu ama ulaghai kwa lengo la unyonyaji zaidi ya hapo Edina ameelimisha kwamba biashara hii haramu ni yapili duniani kwa kuingiza faida.Biashara nyingine haramu kwa kuingiza faida duniani ni ya madawa ya kulevya.Lutengano ameenda mbali zaidi pale alipo alipo fafanua kwamba, madhara makubwa yanayo wakuta wahanga wa biashara hii ya utumwa nikwenda kutumikishwa kingono,kuuawa nakuondolewa baadhi ya viungo vya mwili kama mafigo ,mapafu, ini naviungo vingine ambavyo huko ughaibuni wanavihitaji kwa ajili ya kuviuza kwa wale ambao vyakwao vimekwisha athirika mbaya zaidi ni kwamba wahanga wa utumwa hutengwa na familia zao amesema lutengano. Lutengano amezidi kueleza kuwa biashara ya utumwa inayofanyika humu ndani ya nchi niile ya kwenda kuhamisha
watoto na watu wazima kwa njia ya vitisho ,ulaghai utekaji , kisha kuwapeleka maeneo mengine hasa mijini husuan Dar ,Arusha, Mbeya, Mwanza,Morogoro nk kwa ahadi ya kuwasomesha ,kuwapa ajira,lakini wakisha fika huko huishia kuwa watumwa wangono na kuuzwa kwa wale wanaowahitaji.Lutengano amesema hata hivyo hata hawa wa naofanya biashara ya utumwa humu ndani ya nchi wakinaswa faini ni 50.000.000
Je? Sheria ya kudhibiti biashara hii haramu inasemaje? Kwanza ijulikane kwamba sheria hii ipo ilipitishwa mwezi june 2008 sheria yenyewe infafanua kwamba, adhabu ya anayetiwa hatini kwa kosa hili ni faini inayoanzia shilingi 2000,000 au 50.000.000 au kifungo kisichopungua kuanzia mwaka 1 hadi 7 je? Unawajua magwiji wanao jihusisha na biashara hii ya utumwa Hususan hapa kwetu Tanzania? Imetanabaishwa kwamba, wanaojihusisha na biashara hii ni baadhi ya ndugu wakaribu wa wahanga wa biashara hii ya utumwa ,majirani,wazazi, marafiki, na walezi. Pia imegundulika kwamba,wakati mwingine kinachopelekea ndugu hao kujiingiza katika biashara hiyo haramu ni elimu duni,na tamaa ya kupata mali haraka haraka Je unaijuaFalsafa ya utawala huu wa awamu ya tano ulioko chini ya Mh.J.Magufuri? Falsafa yake inajiweka wazi kwamba ujamaa ndiyo njia sahihi ya kuwafanya watu wajihisi wao ni ndugu,misingi hiyo inasema hivi ,wanadamu wote nisawa.kwamba kila mtu anastahili heshima .kwamba kila raia nisehemu ya taifa na anayohaki ya kushiriki sawa na wengine katika serikali tangu zile za mitaa za mikoa,hadi serikali kuu kwamba kila raia anayo haki ya uhuru wakutoa mawazo yake bila kuvunja sheria ,kwenda anakotaka ,kuamini dini anayotaka,kukutana na watu ilimradi havunji sheria, kwamba kila mtu anayohaki ya kupata malipo kutokana nakazi aliyofanya ,kwamba raia wote wanamiliki utajili wa asili wa nchi hii ukiwa kama dhamana kwa vizazi vijavyo.kwamba ilikuhakikisha kuwa uchumi wanchi unakwenda sawa serikali lazima iwe na mamlaka kamili juu ya njia muhimu ya kukuza uchumi.kwamba ni niwajibu wa serikali ,ambayo ni ya watu wenyewe ,kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi wa taifa ili kuhakikisha ustawi wa raia na kuzuia mtu kunyonya mtu mwingine au kikundi kingine au kuzuia limbikizo la utajiri kufika kiasi ambacho hakipatani na siasa ya watu wote kuwa sawa.Kwa falsafa hii nikwamba njia kuu za uchumi kam Ardhi, misitu,madini,maji,mafuta na nguvu za umeme njia za bahari ,usafirishaji,mabenki ,bima biashara za kigeni,simenti mbolea, nguo , vinatumika kwa maana ya kuwanufaisha wa Tanzania wote.Ndio maana nilianza na na kauli isemayo tusipokua makini tutarudi ukoroni .Unaweza kuona biashara hii ya utumwa ingawa ni haramu lakini wanaonufaika nayo wanaiona kama hakuna njia murua ya kuboresha maisha yao.Mwaka 1888 ilimvuta hata Sultani Khalifa kuja Zanzibar kunufaika na biashara hii ya utumwa Khalfa aliingia kiwewe baada ya mataifa yaliyokuwa wateja wake wakubwa wa kununua watumwa kusain baada ya kusaini mkataba wa kukomesha biashara ya utumwa. Biashara mbayo kwa leo inaratibiwa kwakutumia sayansi ya hali ya juu na kwakutumia ,technolojia mpya,elimu mpya na gharama mpya.ijulikane kwamba Waliokua wateja wa sultani kahalifa wa kununua watumwa walikua Wajerumani,Waingereza,Wataliano,Wareno,wote hawa baada ya mapinduzi ya viwanda kule ulaya walisimamisha biashara hii kwa kutumia viongozi wa dini na sheria ya kuzuia biashara ya utumwa,ingawa sheria ya kupambana na utumwa ilipitishwa na magwiji hao , Lakini Ufaransa iligoma kusaini mkataba huo wao waliendelea kufanya biashara hiyo haramu na sultan Khalifa wazanzibar waliendelea kuuza watumwa katika visiwa vya Ngazija,Shelsheli,Reunion na Madagaska.Hapa Tanzania ninini kitatokea ikiwa magwiji hao wa kuuza watanzania wenzao {watuma} hususan vijana wenye nguvu wakimalizika ambao kwa asili ndio nguzo kuu ya kuzalisha mali kama kilimo ,ufugaji ,uvuvi,nk?
KIBONDO DISTRICT COUNCIL, KIBONDO TOWNSHIP IHULILO STREET
Anuani ya Posta: P.O.BOX 43, KIBONDO
Simu ya Mezani: +255 028 282 0084
Simu: +255 028 282 0084
Barua pepe: ded@kibondodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Kibondodc .Haki zote zimehifadhiwa.