Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo katika kikao chake kilichofanyanyika leo tarehe 28.01.2021 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri (IOM) Kibondo, limejadili na kupitisha Bajeti ya Halmashauri yenye jumla ya TZS.31,034,281,598/- . Katika fedha hizo zinazotarajiwa kukusanywa na kutumika, kiasi cha TZS.16,412,624,000/- ni kwa ajili ya mishahara, TZS.11,375,989,318/- ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo na TZS.3,245,668,279/- ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Mara baada ya kupitisha Bajeti hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mhe. Luis Bura alizungumza na Madiwani, Wakuu wa Idara na Vitengo, Watumishi wa Serikali na Wananchi waliohudhuria kikao hicho.
Katika mazungumzo hayo Mkuu wa Wilaya aliwapongeza waheshimiwa Madiwani kwa kuchaguliwa nakuanza kutekeleza majukumu yao. Alisisitiza juu ya kuendelea kudumisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Vilevile Mkuu wa Wilaya aliwaomba madiwani kutoa ushirikiano katika kusimamia elimu, kilimo, ukusanyaji wa mapato na kutatua kero za wananchi. Katika kilimo alisisitiza juu ya uanzishaji mashamba ya michikichi, maparachichi na kutatua mgogoro katika shamba la miwa ili mwekezaji atakapopatikana pasiwe na usumbufu juu ya uanzishaji wake.
KIBONDO DISTRICT COUNCIL, KIBONDO TOWNSHIP IHULILO STREET
Anuani ya Posta: P.O.BOX 43, KIBONDO
Simu ya Mezani: +255 028 282 0084
Simu: +255 028 282 0084
Barua pepe: ded@kibondodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Kibondodc .Haki zote zimehifadhiwa.